Ukiyazingatia Haya Utaishi Maisha bora ya Kimafanikio

Ni makosa kufikiri muda unaenda. Muda hauendi. Muda upo hapa mpaka mwisho wa dunia. Ni wewe ndo unaenda.

Haupotezi muda, muda hauna mwisho. Unajipoteza mwenyewe, wewe una mwisho. Ni wewe unayezeeka, muda hauzeeki. hivyo tumia mda wako vizuri katika hii dunia.

Namna mbaya sana ya kupoteza muda wako ni kujifananisha na wengine. Ng'ombe anakula majani na ananenepa, lakini Mbwa akila majani atakufa.

Kamwe usijilinganishe na wengine. Kimbia mbio yako. Kinachomfaa mwingine kinaweza kisimfae mwingine.

Tazama zaidi zawadi na kipawa alichokupa Mungu, na usiwe na wivu juu ya baraka walizopewa wengine.

Kama ua rozi linanukia vizuri zaidi kuliko nyanya, haimaanishi kuwa rozi litatengeneza supu nzuri zaidi. Usijaribu kujilinganisha na wengine.

Pia una uwezo wako, utafute na ujijengee uwezo zaidi.

Wanyama wote duniani walikuwa kwenye safina ya Nuhu, na konokono ni mmoja wapo, Kama Mungu aliweza kumsubiri mpaka konokono aingie kwenye safina ndipo afunge mlango, mlango wako wa neema kamwe hauwezi ukafunga kwako mpaka ufike mwisho, siku zote mtegemee yeye utapokea unayostahili.

Kamwe usijidharau, endelea kusonga mbele. Kumbuka kuwa rangi zilizovunjika, bado zinachora kuleta mandhari nzuri ya kuvutia na kupendeza
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment