FAHAMU KUHUSU CHANJO YA MDONDO / KIDERI

Chanjo hii ina virusi hai vya mdondo vinavyotengeneza kinga dhidi ya ugonjwa wa mdondo/kideri. Virusi hivi vimeoteshwa kwenye mayai ya kuku wasiokuwa na magonjwa anuwai.
Chanjo hii inapatikana katika chupa zenye ujazo wa dozi ya kuku 100 na kuku 200.

Hifadhi
Chanjo ya 1-2 imehifadhiwa katika chupa za plastiki ambazo ni rahisi kusafirisha na zina mfuniko wenye sili. Ukishafungua mfuniko mdomo wa chupa unatumika kudondoshea matone ya chanjo kwa urahisi na kwa usafi zaidi.

Utunzaji
Chanjo ya 1-2 inasambazwa katika hali ya majimaji. Chanjo hii ni stahimilivu kwa joto, ikihifadhiwa kama inavyoelezwa hapo kwa njia zifuatavyo;

Chanjo ndani ya jokofu kamwe isiwekwe kwenye sehemu ya kugandishia barafu (freezer), Kama hakuna jokofu, chanjo hii itunzwe kivulini, kwenye hali ya ubaridi na kutumiwa haraka iwezekanavyo.

Hifadhi ya chanjo na muda wa matumizi
Chanjo ihifadhiwe kwenye nyuzi joto kati ya 2-8 (jokofu) muda usiozidi miezi mine, nyuzi joto kati ya 25-30 muda usiozidi siku 7 na nyuzi joto zaidi ya 30 kwa siku 2. Chanjo iliyofunguliwa itumike ndani ya siku 2.

Usafirishaji
Chanjo isafirishwe kwenye hali ya ubaridi ndani ya kasha la barafu lenye barafu, vinginevyo chanjo isafirishwe kwenye chombo baridi kama kasha la karatasi lenye magazeti na barafu au chupa za plastiki za maji ya chumvi nyingi yaliyogandishwa.

Katika hali ya vijijini, chupa yenye chanjo iviringishwe kutambaa cha pamba kilichowezeshwa maji baridi na huku isafirishwe kwenye kijikapu kidogo kilichofunikwa chenye matundu makubwa yapitishayo hewa pande zote.

Matumizi
Chanjo itumike moja kwa moja toka kwenye chupa ya chanjo bila kuchanganya na kitu chochote. Weka tone moja la chanjo kwenye jicho moja la kila kuku.

Muda wa kuchanja
Kuku wa umri wowote wanaweza kupatiwa chanjo. Chanjo ifanyike kila mara baada ya miezi mitatu (3)

Kumbuka
Epuka kuweka chanjo kwenye joto la juu na mwanga wa jua.

Chanjo hii ni kwa kukinga ugonjwa wa mdondo au kideri tu.

Chanja kuku wenye afya tu (Epuka kuchanja kuku wagonjwa).

Hii ni chanjo na wala siyo tiba, hivyo isitumie kuchanja kuku wagonjwa.

Chanjo hii haina madhara kwa vifaranga, wala ukuaji au utagaji wa mayai.

Kuku hupata kinga ya kutosha dhidi ya ugonjwa wa mdondo au kideri siku 7 hadi 14 mara baada ya kuchanjwa.

Kuku wachanjwe kila baada ya miezi mitatu (3).

Dozi (tone moja kwa kuku wa umri wowote (kuanzia kifaranga wa siku moja hadi kuku mzee) au wa jinsia yeyote.

Kama tone halikuingia vizuri kwenye jicho, rudia kwa kuweka tone la pili.

NB; Kwa maelezo zaidi muone mtaalamu wa mifugo aliye karibu na wewe kwa ushauri
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment