Kanuni za ufugaji bora wa mbuzi


Mbuzi ni moja ya wanyama ambao wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu pia ni wavumilivu wa ukame na maradhi tofauti na ngo’mbe kwa kua wana umbile dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na nguvu kazi ndogo na hata kwa wenye kipato kidogo.

Pia mbuzi huzaa (uzao) kwa muda mfupi ili kumwezesha mfugaji kuwa na mifugo mingi kwa muda mfupi. Mbuzi wanaweza kufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi na mazao mengine kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato.

Namna bora ya ufugaji.
Wafugwe kwenye banda bora.
Chagua kulingana na sifa zao na lengo la ufugaji (uzalishaji) nyama au maziwa.
Walishwe chakula sahihi kulingana na umri.
Kuzingatia ushauri wa mtaalamu wa mifugo hasahasa namna ya udhibiti wa magonjwa.
Kuweka kumbukumbu za uzalishaji.
Kuzalisha nyama au maziwa bora yanaokidhi mahitaji ya soko.

Sifa za zizi au banda bora la mbuzi.
Banda bora linatakiwa liwe ni lenye kuweza kuwakinga mbuzi au kondoo na mashambulizi ya wanyama wakali (hatari) na wezi.
Liwepo sehemu ambayo maji hayawezi kutuama.
Mabanda yatenganishwe kulingana na umri.
Liwe na ukubwa ambao linaweza kufanyiwa usafi.

Kama utafuga mbuzi kwa kuwafungia (shadidi) muda wote zingatia yafuatayo:-
Banda imara lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya,upepo/mvua.
Lenye hewa ya kutosha.
Liwe na sakafu ya kichanja na sehemu ya kuwekea chakula na maji.
Liwe na vyumba tofauti kwa kuweka vijitoto/wanao ugua/wanao kua.

 Ujenzi wa banda la mbuzi.
Banda lijengwe kwa kutumia vifaa vilivyopo eneo husika na kwa kuzingatia uwezo wa mfugaji.
Kuta ziwe imara na zinazo ruhusu mwanga na hewa ya kutosha.
Mlango uwe na ukubwa wa 60X150 sentimeta.
Sakafu iwe ya udongo/zege ya kichanja unaweza kutumia mabanzi/mianzi na iruhusu kinyesi na mikojo kudondoka chini.
Chumba cha majike na vitoto kiwe na sentimeta 1.25kati ya fito na fito au papi na papi, chumba cha mbuzi wakubwa kiwe na sentimeta 1.9 kati ya mbao na mbao.

Ansante kwa kuwa nasi katika makala haya ya ufugaji, usikose sehemu ya pili ya somo lijalo jinsi ya kuchagua mbegu bora ya mbuzi wa kuwafuga.
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment