Ifahamu vizuri Biashara ya Kuuza Matunda, Jinsi inavyolipa


             
🔴UTANGULIZI
Biashara hii ni miongoni mwa zile biashara zenye kuhitaji mtaji kidogo na huwa na faida kubwa ya haraka.

Mitaani matunda kama maembe, mapapai machingwa, Nanasi, tikiti maji, parachichi, ndizi na mabungo ni miongoni mwa matunda muhimu yanayopendwa zaidi na jamii ya watanzania.

Matunda hutofautiana upatikanaji kuendana na msimu na msimu. kuna msimu embe zinakua nyingi, kuna msimu wa machungwa, msimu wa nananasi no

🔴BAADHI YA MASOKO MAKUU YA MATUNDA
Kwa Dar e's salam matunda hupatikana kwa wingi
         ➡ Soko la ilala
         ➡ Stirio Temeke
         ➡ 

Bagamoyo 
        ➡ Magomeni sokon
        ➡ Soko jipya 
(Tutawaletea orodha mikoa yote katika makala zijazo)

🔴 AINA ZA KUIFANYA BIASHARA HII NA MTAJI WAKE
Kuna njia kuu.mbili za kuifanya hii biashara 
i/- kukodisha fremu na kuuza 
ii/- kutembeza na toroli mtaani 

🔴MAKADIRIO YA FAIDA 
Matunda mara nyingi huuzwa mara mbili ya bei ulonunulia ( faida = 50%).kipindi cha msimu wa matunda husika mfano: msimu wa machungwa, bei ya jumla huuzwa sh.80 kwa kila moja nawe utaenda kuuza sh.150 au sh.200 kuendana na eneo husika.

Kwahiyo: ukianza na mtaji wa sh.50,000 kununua matunda utazalisha wastani wa sh.30,000 faida baada ya mzigo kuisha (Assume matunda yenye thamani ya sh.20,000 yameharibika). 
NB: Kumalizika kwa mzigo hutegemea na uchangamfu na uhai wa biashara yako. Wapo wenye wateja wengi ambao kwa siku huuza matunda yenye wastani wa sh.200,000 nk

🔴CHANGAMOTO ZA BIASHARA
👉kuoza kwa matunda
👉kubadilika kwa misimu ya upatikanaji matunda
👉Mabadiliko ya mara kwa mara yasio rasmi ya bei za matunda.

🔴JINSI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO
👉Tengeneza wateja wa uhakika kabla ya kuchukua mzigo.mkubwa wa matunda ili kuepuka matunda mengi kuozea dukani.
👉Tengeneza chaneli kubwa na wafanyabiashara wenzio ili kufahamu mabadiliko na msimu ya matunda husika

#SED4LYF
                          @sharak
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment