Habari rafiki, Karibu katika wasaa huu wa kujifunza na kuelimishana juu ya mambo mbalimbali katika maisha yetu ili tuweze kufikia mafanikio yale tunayoyataka.
Leo tutajadili Kujifunza kama moja ya njia mojawapo za kufikia mafanikio. Ndio ni njia mojawapo ya kufikia mafanikio kwa sababu inakufanya unakuwa bora katika taaluma uliyonayo kwa kuongeza kitu kipya ambacho haukuwa nacho ambacho kinaenda kuboresha kile ambacho umechagua kufanya hivyo unakuwa mbobezi wa taaluma hiyo.
Bila shaka unajua ya kuwa kujifunza ni tendo endelevu, yaani halina ukomo. Hata kama umemaliza masomo katika ngazi yoyote ya elimu hata iwe ya chuo kikuu na ukapata shahada ya juu kabisa ya uzamili, bado utahitaji kujifunza ili uwe bora katika eneo lako la kazi ulilosomea au unalofanyia kazi na hatimae utakuwa mbobezi ambae hutatatereka katika jambo ambalo huenda hukuwahi kufundishwa lakini kupitia kujifunza nje ya mfumo wa elimu utaweza kukutana na elimu ambayo itakusaidia kutatua mambo kama hayo usiyoyatarajia.
Hivyo kujifunza ni jambo jema na lenye manufaa kwa mtu yeyote. Kuna njia nyingi za kujifunza mambo mbalimbali katika maisha yetu. Mara nyingi tumekuwa au tumezoea kujifunza katika mfumo wa elimu rasmi – yaani unaingia darasani na kufundishwa kile kilichopangwa na mfumo.
Lakini mfumo huu umekuwa na mapungufu katika baadhi ya mambo kwani haukidhi mahitaji ya yule anaejifunza hivyo kukosa uhalisia kabisa, hivyo kuna njia za ziada ambazo mtu peke yake na kwa wakati wake anaweza kujifunza na akaweza kujielimisha zaidi na kuwa mtaalamu kabisa asietiliwa shaka na elimu hiyo atakayokuwa ameipata au kwa msaada wa wengine pia unaweza kujifunza kama nitakavyokueleza hapo chini.
Hii itathibitishwa na thamani na ubora wa kazi atakazokuwa akifanya. Hebu tuangalie baadhi ya njia ambazo unaweza kutumia kujifunza wewe peke yako au kwa msaada wa wengine na kupata maarifa ambayo yatakufanya kuwa bora katika eneo lako.
Kusoma; Njia hii ni nzuri na ya uhakika katika kujifunza, njia hii itakufanya uwe bora katika chochote kile ulichochagua kufanya katika maisha yako. Cha msingi angalia umechagua nini na tafuta vitu vya kusoma katika eneo hilo ulilochagua kulifanya katika maisha yako. Vitu vya kusoma vipo vingi sana katika dunia hii hususani katika wakati huu wa mapinduzi ya taarifa na teknolojia ya habari na mawasiliano – TEHAMA.
Hivyo kuna vitabu vinavyohusu mambo mbalimbali kuanzia biashara, sanaa, siasa, uchumi, sayansi na teknolojia na hata uhalifu kama unataka kujifunza vitabu vipo ili mradi wewe umechagua kujifunza eneo lipi na tafuta kinachokufaa na usome hakika utaongeza maarifa mno na hakuna atakae kuwa sawa na wewe hata kidogo yaani utakuwa wa moto kuliko kawaida! Pia kuna majarida, makala unaweza kusoma na kujielimisha na mitandao mbalimbali ambayo unaweza kusoma na kuifatilia ambayo itakusaidia kukufundisha na kukupa elimu nzuri ya kile unakitaka. Muhimu tu ni kwamba hakuna sehemu utakuta vitu vizuri ukakosa vitu hasi au vibaya hivyo kama utaingia mitandaoni tafuta kile unakitaka tu mengine achana nayo kwani yatakupotezea muda na yatakupa fikra hasi.
Kusikiliza; kusikiliza ni kitendo cha hiari cha kuruhusu akili kuwa makini kusikia kile ambacho unataka kusikia. Tofauti na kusikia, unaweza ukawa unasikia kelele za muziki lakini hausikilizi kwa sababu hujawa makini kuusikiliza na hutazielewa kelele hizo, hivyo ili kusikiliza unahitaji uhiyari au utayari na umakini kusikia jambo fulani. Ili kujifunza unahitaji pia mbali na kusoma, kusikiliza makala za sauti ziliandaliwa na wataalamu katika jambo ambalo unahitaji kujifunza, pia kuna vitabu vilivyosomwa kwa sauti ambavyo unasikiliza na kupata maarifa katika eneo lako la kazi na hatimae kuwa bora zaidi.
Kutazama video za mafunzo; hii ni njia nyingine pia ambayo unahitaji kuitumia katika kujifunza ili kujiongezea maarifa na kuwa mwenye ufanisi. Hapa utaangalia video nyingi kutoka kwa wataalamu katika eneo unalolifanyia kazi. Video hizi unaweza kununua mikanda au CD za mafunzo au kwa kuingia mtandaoni (www.youtube.com) na kutafuta video ya kitu unachohitaji na utajifunza vizuri zaidi.
kuhudhuria semina au warsha za mafunzo; kuna semina au warsha ambazo huwa zinatolewa na watu waliobobea katika taaluma fulani, hivyo ikitokea umepata fursa hiyo itumie kwa kujifunza kwani itakusaidia kuwa bora katika eneo unalofanyia kazi. Semina au warsha hizi kuna za kulipia na za bure hivyo angalia zile zinazokufaa kulingana na hali yako uhudhurie, lakini za kulipia ni nzuri zaidi kuliko za bure.
Tafuta mtu ambae utakuwa unamfuatilia ambae ana ujuzi na uzoefu ambao amekuzidi katika taalauma yako na utakuwa unajifunza kutoka kwake, huyu atakuwa mwalimu wako. Hapa unaweza kuwa nae mmoja au wengi na unaweza kujifunza kutoka kwake au kwao kwa njia mbalimbali.
Kama unaweza kuwasiliana nae moja kwa moja ni vizuri zaidi lakini kama haiwezekani tafuta njia nyingine ambazo ni kupitia maandiko yake kama huwa anaandika katika mitandao au video katika mitandaao hiyo pia unaweza kusoma vitabu vyake kama ni mwandishi au kuhudhuria semina zake au warsha anazofundisha. Kwa njia hii utakuwa nae karibu na utakuwa ukijifunza kutoka kwake mengi sana ambayo yatakufanya kuwa bora zaidi. Kama awali nilivyosema unaweza kuwa nao watu hawa wengi ambao utakuwa ukijifunza kutoka kwao na utakuwa ukipata uzoefu wao kwa utofauti ukiwa nao wengI.
Rafiki hizo ndio njia za wewe kuweza kujifunza katika kile ambacho umechagua kukifanya katika maisha yako ili uweze kufanikiwa. Hivyo utafikia yale ambayo umepanga kufikia na kufanikiwa kwa ujumla katika eneo lako kwani utakuwa bora zaidi wala hakuna changamoto ambayo itakurudisha nyuma.
Kama umejifunza kitu na ungependa rafiki zako nao wapate elimu hii ruksa kuwashirikisha, bonyeza kitufe cha share hapo chini kwenye mtandao unaotaka rafiki zako uwashirikishe na uwashirikishe, kumbuka kushirikishana ni kujaliana hivyo waonyeshe kama unawajali rafiki zako

0 comentários:
Post a Comment