Vitu vya Kufahamu Wakati wa kutoa Chanjo kwa Kuku

Changamoto za kiufugaji ni nyingi ila zisikukatishe tamaa ukifuata kanuni na taratibu za Ufugaji unaweza ukasahau kabisa kama kuna changamoto hizo.

Moja wapo ya kitu cha muhimu kwa kuku wako ni chanjo, chanjo ni kitu muhimu ili kuwafanya kuku wapo wasipatwe na magonjwa hatari kama mdondo( mdonde) , Ndui nk.

Pia ni moja kati ya vitu vya muhimu kwa kuku vitakavyofanya ufuge kwa amani na kusahau changamoto.

Ukizingatia chanjo pia itakuwa rahisi wewe kufikia ndoto zako za kiufugaji, kwani ili kuku wazaliane na mradi wako ukuwe ni lazima udhibiti vifo, kwa kupawa kuku wako chanjo utadhibiti vifo visivyo vya lazima.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kutoa chanjo kwa kuku

  • Hakikisha unazingatia kwa makini masharti ya mtengenezaji wa chanjo: jinsi ya kuhifadhi, kutayarisha na njia inayotumika kumchanja kuku. Wakati wote zingatia masharti ya mtengenezaji kuhusu uhifadhi wa  chanjo ili isipoteze nguvu.
  • Fuata ushauri wa daktari wa mifugo unapoandaaa ya chanjo.
  • Watoa chanjo wapatiwe mafunzo ya jinsi ya kutayarisha na kutoa chanjo
  • Chagua aina ya chanjo kulingana na umri na hali ya kiafya ya kuku.
  • Fanya usafi wa mara kwa mara katika mabanda ili kupunguza wingi wa vimelea kwenye mazingira.
  • Tumia maji ambayo hayajawekwa dawa au kemikali kwa ajili ya kuchanganyia chanjo, k.m. maji ya kisima, mvua, n.k. Maji ya kuchanganyia chanjo yawe na ubaridi, yasiwe moto.
  • Changanya chanjo kabla ya kutumia na iwekwe mbali na kuku.
  • Pata ushauri wa daktari wa mifugo kabla ya kuchanja kuku wagonjwa au wale ambao hawako katika muonekano mzuri
  • Siku ya chanjo, usiwape kuku maji kwa masaa 3 – 4 ili waweze kunywa maji yaliyowekwa chanjo kwa haraka.
  • Zoezi la uchanjaji lifanyike haraka ili kupunguza usumbufu kwa kuku.
  • Tenganisha kuku waliochanjwa na wale ambao hawajachanjwa.
  • Baada ya kuchanjwa, kuku wawekwe kwenye banda linalopitisha hewa vizuri
  • Baada ya kila zoezi la kuchanja, wafanyakazi wabadilishe mavazi, viatu/buti zisafishwe na kuwekwa dawa, na vifaa vilivyotumika viwekwe dawa ya kuua vimelea.
  • Weka kumbukumbu za uchanjaji vizuri


Mambo ambayo hutakiwi kufanya wakati wa utoaji chanjo
Kumwaga chanjo ovyo na kuchafua mikono au nguo
Kuchanganya chanjo za aina mbili au zaidi, isipokuwa pale tu mtengenezaji wa chanjo atakavyoagiza hivyo, au kwa ushauri wa daktari wa mifugo.
Kutumia chanjo iliyopita muda wake
Kutumia chanjo iliyobaki ili itumike kwa kazi ya siku nyingine
Kuchanja kuku ambao wamepatiwa dawa aina ya antibiotiki.
Kuchanja zaidi ya chanjo moja kwa wakati, iwapo haikuagizwa hivyo
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment