Kati ya kuanzisha na kuendeleza ni rahisi sana kuanzisha biashara kuliko kuiendeleza kwa sababu hayo ni mambo mawili tofauti. Tunapozungumzia kuanzisha ni pale biashara yako inapozaliwa lakini kuendeleza tunazungumzia maisha halisi ya hiyo biashara.
Unapoanza biashara unatarajia biashara hiyo kuishi, biashara ina maisha kwa hiyo inaweze kukua na pia inaweza kudumaa na kitu chochote chenye maisha kinaweza kuishi na pia kinaweza kufa.Hakuna mtu anaeanzisha biashara akitarajia biashara hiyo kufa.
Ni jambo la heshima sana kuanzisha biashara ambayo itaweza kuishi kwa muda mrefu,wakati wako na hata kuwaachia kizazi chako kikiiendeleza,kwa sababu zipo biashara nyingi ambazo zinakufa kabla ya kufika mbali.
Karibu tena msomaji wetu katika mtandao wetu wa maishanifursa. Leo tutajikita katika mada ambayo nimeipa kichwa “MAMBO MATATU KUKUSAIDIA KUENDELEZA BIASHARA YAKO ” Nakushukuru sana kwa kuendelea kufuatilia kazi zetu uwepo wako ni muhimu sana kwa kazi yetu kwani bila wewe kazi yetu haina maana.
Watu wengi wana shauku ya kuanzisha biashara lakini hawana picha au sura ya biashara yenyewe itakavyokuwa katika kipindi cha mwaka mmoja,miaka mitano,miaka kumi au hata miaka thelathini ijayo.
Huna haja ya kusubiri ukamilike kwanza ndipo uendeshe biashara kwa mafanikio, usingoje mpaka uwe kamili kabisa lazima uwe na nafasi kuanzia mahali fulani na kuboresha kadri unavyoendelea. Wafanyabiashara wenye mafanikio wameumbwa kama wewe na kujiendeleza katika kile wanachoamini kufanya kwa sababu,maendeleo ni mchakato wa kujifunza usio kuwa na mwisho.
Yapo mambo ambayo utajifunza vizuri sana kabla hata ya kuanzia lakini yapo mambo ambayo huwezi kabisa kupata nafasi kujifunza mpaka umepata mpenyo wa kuanzisha na kuendesha biashara. Nadharia anaweza kukufundisha mtu kwa urahisi lakini kupata uzoefu unahitaji kuanza kuweka kwenye matendo yale uliyojifunza kwa nadharia.
Changamoto na mapungufu utakayokutana nayo wakati unaendelea kuishi katika biashara na namna utakavyoyashughulikia kupata majibu ya hizo changamoto.ndicho kitu kitakachokutofautisha na kukupa uzoefu wa kuendesha biashara. Hakuna anaeweza kukufundisha changamoto ila tunakitana nazo tukiwa kazini.
Ili kuwa na biashara endelevu lazima uwe na maarifa ya kuendesha biashara na huwezi bila kuwa na taarifa sahihi zitakazokusaidia kufanya maamuzi mara kwa mara kuboresha biashara yako. Yapo mambo machache ambayo unapaswa kuyajua kama unataka kuendesha biashara yako kwa mafanikio makubwa.
Mambo matatu muhimu kukusaidia kuendeleza biashara yako;
Fuatilia kwa ukaribu pesa yako.
Kwa kuwa mada yetu leo inazungumzia namna ya kunedeleza biashara hatutazungumzia kwa undani habari ya kuanzisha biashara. Kupitia makala hii tunazungumzia zaidi biashara ambayo tayari imekwisha aanza. Kufuatialia fedha yako kwa ukaribu ni kitu muhimu sana ambacho kila mfanya biashara anapaswa kukizingatia. Kuna msemo wa Kiswahili ambao husema biashara bila daftari hupotea bila habari.
Kama wewe unafanyabiashara lakini huwezi kabisa kufuatilia pesa yako pasi kifo cha hiyo biashara kiko jirani sana. Biashara yoyote ina milango miwili ule wa kuingiza na malango wa kutoa. Unapaswa kufuatilia milango yote miwili ya fedha yako. Fedha inayoingia na fedha inayotoka yote ni muhimu. Kujua mlango unaokuingizia pesa na mlango unaotoa pesa yako ni kitu cha msingi sana kufanya. Kuishi bila kujua pesa yako inavyoingia wala inavyotumika ni hatari kama mgonjwa kuumwa bila kutafuta tiba.
Wafanya biashara wengi waliojikuta wanaingia kwenye hasara kubwa na pengine kupoteza kabisa biashara zao wameingia katika jaribu la kuuza na kutumia pesa moja kwa moja bila kuweka kumbukumbu. Ili mradi pesa inaingia wanatumia moja kwa moja, na kwa namna hiyo kamwe hawawezi kuwa na taarifa juu ya mambo yanayoendelea kuhusiana na pesa zao kwenye biashara.
Hatua hii inakusaidia kubaini kiasi cha pesa inayoingia kupitia vyanzo vyako na pia mambo yanayoteketeza pesa yako. Utahitaji kuboresha kila siku biashara yako iwe upande wa maingizo au hata upande wa matumizi pia. Bila kuweka kumbukumbu hakuna namna unaweza kuboresha biashara yako.
Tengeneza taarifa
Kuwa na habari bila kuzitumia ni karibu sawa na kutokuwa nazo kabisa. Habari ni muhimu tu wakati utakuwa na uwezo wa kuzitumia na hivyo kusaidia kufanya uamuzi sahihi wa kuboresha biashara yako. Kuwa mtu wa kutoa taarifa kwenye biashara yako.
Taarifa za vipindi mbalimbali za biashara yako zitakusaidia sana kuboresha na kukuza biashara yako. Hatua ya kuweka kumbukumbu itakusaidia sasa kuandaa taarifa ya biashara yako kila siku, kila wiki, kila mwezi na kila mwaka wa fedha. Taarifa utakazozipata kutokana na utunzaji wa kumbukumbu za maingizo na matumizi kwenye biashara yako zitakusaidia sana katika hatua ya kuandaa taarifa za fedha katika vipindi mbalimbali.
Taarifa hizi zitakusaidia kujua kiasi cha pesa uliyoingiza na ile uliyotumia kulingana na makisio uliyojiwekea. Je matumizi yako yenaendana na makisio uliyojiwekea. Pengine matumizi yamekua juu sana kiasi cha kusababisha kupunguza faida yako utaanza kujiuliza. Je nifanye nini ili kupunguza matumizi yasiyokua ya lazima na kupunguza gharama? Je Mapato yamepungua nifanye nini ili kuongeza mapato na kufikia lengo?
Itakusaidia sana kuwa na picha halisi ya biashara yako na kuona mwenendo unaopaswa kwenda nao kuimarisha biashara yako. Mfanya biashara unahitaji kufanya maamuzi ya mara kwa mara kuboresha biashara yako na pale unapokua na taarifa ya kile kinachoendelea kwenye biashara utaweza kufanya maamuzi sahihi.
Tafuta maarifa.
Moja ya sifa muhimu ya mfanya biashara anayopaswa kuwa nayo ni kujifunza kila siku bila kukoma. Mfanyabiashara ambaye tayari yeye amekwisha kufunga kabisa mlango wa kujifunza huyo hawezi kuwa na nafasi kubwa kwenye maisha ya uendeshaji wa biashara yake.
Katika dunia ya sasa ya utandawazi zipo njia nyingi na rahisi kujifunza maarifa mengi ikiwemo maarifa juu ya biashara. Zama hizi unaweza kujifunza sana kupitia mtandao wa intaneti. Hakuna kitu utakachotaka kujifunza ukakosa cha msingi ni kujua tu unachotaka kujifunza. Kuna waalimu wa kila aina kwenye mtandao ambao unaweza kuwafuatilia na kujifunza kutoka kwao.
Jifunze ujuzi unaohitaji.
Kuna njia nyingi sasa ambazo mtu anaweza kujifunza kitu kipya nyakati za leo kuliko kipindi chochote ambacho dunia imepita. Elimu nyingi zinapatikana kwenye mtandao ingawa wakati mwingine unahitaji kuwa makini unapotumia njia hii ya kujifunza. Unaweza pia kuhudhuria semina za muda mfupi juu ya maarifa unaohitaji, kusoma vitabu au kujiunga na darasa kamili ya muda ili kupata maarifa unayohitaji kuendesha biashara yako.
Ajiri watu wenye ujuzi wakusaidie
Huhitaji kujifunza kila kitu ili uweze kuwa mfanya biashara uliyefanikiwa hapana. Yapo mambo ya msingi ambayo utaweka nguvu kubwa kujifunza na yapo yale ambayo utalazimika kutafuta namna nzuri ya kutumia maarifa ya watu wengine.
Inawezekana ukawa na taarifa juu ya ujuzi ambao unahitaji ili kuendesha biashara yako lakini huo ujuzi huna wala huwezi kusomea kila kitu. Njia rahisi ya kutatua changamoto hiyo ni kutafuta watu wenye maarifa ambayo huna ili wakusaidie kuendesha kwa kutumia maarifa yao kwa kuwalipa. Hakuna anaeweza kufanya kila kitu peke yake.
Dunia imejaa watu wenye ujuzi katika maeneo mbalimbali ya taaluma wanatafuta mahali pa kuajiriwa. Njia rahisi ni kuajiri kwa muda ama moja kwa moja kutegemeana na ukubwa wa biashara na mahitaji yako.
Naamini utakuwa umepata kitu kupitia makala hii fupi. Ukiwa na uhitaji wowote au ushauri katika eneo lolote la kuboresha maisha yako usisite kuwasiliana nasi kupitia njia za mawasiliano hapo chini. Aidha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno, whatsapp kupiga simu au kututumia barua pepe nasi tutarudi kwako mapema iwezekanavyo

0 comentários:
Post a Comment