BIASHARA YA KILIMO CHA MCHICHA NA KANUNI ZAKE

Mchicha ni mboga za majani ambazo zina faida lukuki katika miili yetu. Ukiachilia mbali faida hizo pia kilimo cha mchicha kina faida lukuki hasa pale mtu anapoamua kujiweza katika kilimo hiki. Kilimo hiki ni kizuri kwa sababu huwa hakichukui muda mwingi katika upandaji hadi uvunaji.

Hali ya hewa na udongo kwa  kwa ajili ya ulimaji wa kilimo hiki.
Mchicha unahitaji maji ya kutosha katika kipindi chake chote cha ukuaji hadi kuvuna. Vilevile mchicha huhitaji udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye kuhifadhi maji.

Utayarishaji wa shamba.
Tengeneza shamba la mchicha kwa kutifua ardhi na kulainisha udongo wenye kina cha sentimeta thelathini. Weka mbolea ya samadi debe moja katika kila mita moja ya mraba. Panda mchicha katika matuta yenye upana wa 90cm-100cm.

Aina za mbegu
Amaranthus hybridus huu ni mchicha wenye majani mekundu na mbegu zake ni nyeusi.
Amarantus africana ni mchicha wenye majani ya kijani na mbegu zake ni ni nyeusi.
Amaranthus hypochondriacus ni mchicha wenye majani ya kijani na mbegu zake ni njano hasa mbegu zake hutumika kutengeneza uji wa watoto wachanga.
Amaranthus dubius ni mchicha wa kienyeji na Aspinosus ni mchicha wenye miba mingi.

Upandaji
Mchicha upandwe katika tuta kwa mistari yenye nafasi ya sentimita thelathini.
Funika mbegu kwa kutumia udongo uliolaini na tandaza nyasi kavu baada ya kupanda ili kutunza unyevunyevu na toa matandazo baada ya siku tatu hadi tano tangu siku ya kupanda.
Pandikiza mchicha kwa nafasi ya sentimeta kumi na tano kwa ishirini.
Mwagilia maji ya kutosha.

Namna ya kukuzia.
Tumia mbolea ya samadi iliyolowekwa kwenye maji kwa muda wa masaa ishirini na nne kumwagilia mchicha wako ili kupata mavuno mengi zaidi. Tumia kiasi cha debe moja kwa kila mita moja ya mraba.

Namna ya kudhibiti wadudu waaribifu.
Adui mkubwa wa mchicha ni wadudu aina ya mafuta au kitaalamu zaidi huitwa spinach aphids ambao hufyonza utomvu wa mchicha na kusababisha majani kujikunja , mchicha kusinyaa na kunyauka. Kudhibiti wadudu hawa mwagilia mchicha wako kutumia chombo kinachotoa maji mithili ya mvua kitaalamu kinaitwa "watering can" ili kuwadondosha wadudu hao.

Wadudu wengine ni kitambazi ambacho hula majani ndani kwa ndani hivyo tumia mwarobani kunyunyuzia majani ili kuwaua wadudu hao waharibifu.

Mavuno
Mchicha huwa tayari kuvunwa baada ya majuma 3 hadi 6 tangu kupandwa au kupandikizwa. Uvunaji huweza kuendelea kwa muda wa miezi 2 hadi 3 kutegemeana na namna utakavyoamua kuuvuna mchicha wako.

Kiasi cha mavuno


Kila mita moja ya mraba huzalisha kiasi cha 4kg hadi 5kg za mchicha. Hii inamaanisha kuwa utapata kiasi cha tani 20 hadi 40 kwa hekta moja ya mchicha
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment