MAMBO YA KUZINGATIA PALE UNAPOANZISHA BIASHARA

Njia pekee itakuyokusaidia kuingiza kipato cha ziada na kukupeleka kwenye uhuru wa kifedha ni kwa wewe kuamua kuanzisha biashara yako na utakayoamua kuisimamia kikamilifu hadi ikuletee mafanikio.

Ili kuanzisha biashara na ikafika mahali ukaanza kuona matunda ya biashara yako, kwa kawaida huwa ipo misingi au mambo ambayo unatakiwa uzingatie sana ili biashara yako iweze kudumu na kutoa faida uitakayo.

Yafuatayo Ni Mambo Ya Kuzingatia Pale Unapoanzisha Biashara.

 1. Elewa wateja wako wa mwanzo wanataka nini na hapo utapata picha ya jinsi utavyoiendesha biashara na uzingativu juu ya kazi. Ukijua wateja wako wanataka kitu gani, itakusaidia sana kuweza kuwapa huduma hiyo.

2. Kuwa mbunifu,  hilo ndilo jambo kubwa zaidi, biashara ni zilezile ila kinachofanya wateja wakimbilie biashara  yako ni ubunifu wako. Kama usipokuwa mbunifu na ukataka kufanikiwa kibiashara uwe na uhakika utakwama.


3. Lugha nzuri kwa wateja na ukarimu, huweza kumasisha kuongezeka wa wateja wengi katika biashara yako. hakua biashara ambayo italeta mafanikio makubwa kama wewe mwenyewe una lugha mbovu na wateja wako.

4. Epuka kutoa pesa ya mtaji kwa mahitaji binafsi utaua biashara. Hakikisha mahitaji ya biashara na mahitaji yako binafsi unatenga kabisa. ni sumu kubwa sana katika biashara kama eti huwezi kutofautisha matumizi binafsi  na biashara yako.

5. Jenga utaratibu wa  kufanya tathimi ya biashara yako wapi ulipotokana wapi ulipo na wap unaelekea,? Je, unasonga mbele au unarudi nyuma, ukiona unarudi nyuma jiangalie upya, kujitathimini na ushituke mapema kabla jahazi halijazama.

6. Hifadhi kumbukumbu, hasa matumizi pamoja na mapato hata ya shilingi moja ya sehem ya biashara. Jambo ambalo watu wengi hasa sisi weusi ni ngumu kwetu, na hii ni kila siku unatakiwa kufanya. Huwezi kuendesha biashara na  ikakua bila ‘documentation’. Hutajua ulikotoka, ulipo na unako enda kibiashara.

7. Kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali wanaofanya biashara kama yako na kufanikiwa pia usiwapuuze walioshindwa kwani nao wanacho cha kukufundisha. Jifunze kwao kila siku hadi uweze kufanikiwa.

8. Kuhakikisha biashara/duka haliishiwi bidhaa na kama likiishiwa bidhaa maana yake uliowakopesha hawajarudisha, pia jitahidi kuweka mambo, mazingira ya kuvutia wateja. Ukiweka mazingira hayo ujue ni lazima utaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

9. Kujitahidi kuweka aina ya bidhaa ambazo wateja wako watapata kwa urahisi na jamii itakayo kuzunguka. Mteja anapenda sana duka ambalo kila akienda hakosi bidhaa ambayo anaihitaji. Hapo ndipo mahali pake.

10. Jitahidi na jifunze kukubali challenges/changamoto  katika biashara yako na kutafuta njia madhubuti ya kuzimaliza au kuzishughulikia. Ukiwa mtu wa kulia na hutaki changamoto uwe na uhakika hutafika popote.

11. Jitahidi kuangalia mbele kadri unavyona faida inaongezeka, jitahidi kuongeza mtaji na kuzid kupanua biashara, hata kwa kufungua matawi zaidi pengine na kuongeza ubora na ufanisi.

 12. Usafi, ukarimu, kusoma nyakati, utafiti na ubunifu na ni moja pia ya mambo ya kuzingatia. Eneo lako la biashara likiwa safi na ukaongeza na ukarimu ni lazima utawavuta wateja wako katika biashara kwa sehemu kubwa.

Kama unataka kuanzisha biashara na ikakupa faida, hayo ndiyo mambo ya msingi sana unatakiwa kuyazingatia na kuyatilia maanani kwa kiasi kikubwa ili kupata mafanikio makubwa katika biashara yako.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa kibiashara.

Ni wako rafiki katika mafanikio,

IMANI NGWANGWALU
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment