Jambo muhimu la Kuzingatia katika kuyasaka mafanikio

Kabla sijajikiita katika kiini cha somo letu la leo, nataka tujiulize, hivi ili uweze kufanikiwa katika maisha yatu inatupasa tushughulike na nini hasa? nini ambacho huwa kinakuja katika kichwa chako hasa pale ukiambiwa kuhusu mafanikio?

Binafsi niliwahi kufanya uchunguzi usio rasmi kuhusu mafanikio, nikagundua ya kwamba fikra na mtazamo ya watu wengi juu ya neno mafanikio unagemea zaidi katika mitazamo hasi.

Wapo baadhi ya watu wengi huamini, wao huamini ya kwamba, kufanikiwa ni bahati ya mtu mwenyewe, lakini wapo baadhi ya watu wengine wao huamini ya kwamba mafanikio ni uchawi, huku wakiamaini ya kwamba huwezi kufanikiwa bila kujihusisha na masuala ya kishirikina. Kwa maneno mengine tunaweza tukasema ya kwamba mafanikio yana mitazamo mingi sana katika vichwa vya watu.

Lakini ukweli ni kwamba neno mafanikio ni Baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu, ambapo Baraka hizo hujengeka katika kuamini ya kwamba mafanikio yako yanakuja kwa kuaamini njia sahihi za kuleta mafanikio hayo na si vinginevyo.

Hivyo ili uweze kuyapata mafanikio hayo inakupasa ushughulike na fikra. Fikra ndio kitu cha kwanza ambacho unapaswa kushughulika nacho katika kuyasaka mafanikio hayo. Tuposema neno fikra, tunamaanisha fikra chanya.

Au kwa maneno mengine ili uweze kufanikiwa katika maisha yako ni lazima uweze kushughulika na mtazamo wako juu ya maisha yako. Swali la kujiuliza ni kwamba ni nini mtazamo wako juu ya mafanikio?

Endapo majibu ya swali hilo ni mtazamo hasi, basi jifunze kila wakati kuwa na mtazamo chanya, kwani endapo utajifunza kuwa na mtazamo chanya kutakufanya uweze kupiga hatua za kimafanikio.

Mwisho nimalize kwa kusema ya kwamba ukitaka kufanikiwa katika maisha yako hakikisha unashulika na fikra, kwani fikra sahihi ndio kiwanda cha kutengeneza maisha yako.
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment