Jinsi unavyoweza Kufanikiwa katika Maisha yako

Moja ya imani kubwa niliyonayo ni kwamba: kila mmoja wetu anaweza kuwa vile anavyotaka kuwa, tunaweza kuwa tutakavyochagua kuwa. Mafanikio katika maisha ni haki yetu ya kuzaliwa. Na chochote kile tunachokitaka kwa namna moja au nyingine tunaweza kuwa nacho. Ila wengi wetu kwa kutokulitambua hili, tumekuwa  tukidhani kwamba; hatuna kile kinachohitajika ili kwa pamoja tuweze kufanikiwa.

Narudia tena: mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa, na unaweza kuwa vile unavyotaka kuwa bila ya kujari hali yoyote uliyonayo sasa. Na unaweza kulidhibitisha hilo kwa kutazama kila kitu kinachokuzunguka. Na mfano wa vitu hivyo ni kama vile ;kiti, meza, ndege,ghorofa,gari,simu,kompyuta,na gunduzi kadha wa kadha zilizopata kufanywa. Hivi ulikwishawahi kujiuliza, iliwezekanaje kwa gunduzi zote hizo kuja kufanikiwa?Just hang on and i’ll get you there.!!

Kila kitu kilichofanikishwa,au kile kitakachokuja kufanikishwa, ni lazima kitakuwa kimepitia, au  kitapitia uwekezaji wa aina fulani.Je, ni uwekezaji wa aina gani huo?.kila kitu tunachotaka kukifanikisha iwe katika maisha au biashara ni lazima kihusishe mambo makuu matatu. Na mambo hayo ni ;

1. Wazo.
2. Muda.
3. Nguvu.

Mafanikio katika nyanja yoyote ile ni lazima yapitie hatua hizo tatu.kwa mfano; wakati unapotumia zaidi ya miaka 5 katika kujifunza kuhusiana na madawa pamoja na tiba, ni nini hasa unachotarajia kukipata katika maisha yako?. Jibu la swali hilo ni kwamba kwa namna moja au nyingine ni lazima utakuwa daktari. Na wakati unapotumia zaidi ya miaka 5 katika kuangalia TV, kufatilia udaku na umbea. Ni nini hasa unachotarajia kukipata katika maisha yako? Na jibu la swali hilo ni kwamba; hutopata chochote kile chenye manufaa katika maisha yako.Unapoyatumia maisha yako katika mambo yasiyo ya maana, basi usitarajie kupata kitu chochote kile kilicho cha maana.

Ukweli ulio wazi ni kwamba:Namna ulivyoyatumia mawazo yako,muda,na nguvu zako hapo kabla ndiko kulikokufikisha hapo ulipo sasa. Na kesho yako kwa namna moja au nyingine itakuja kujengwa kutokana na jinsi unavyoyatumia mawazo yako,muda ,na nguvu zako sasa.Hakuna kitu cha bure katika maisha.Hakuna njia ya mkato katika mafanikio.Mafanikio ya haraka haraka huwa yanazeeka haraka.Chochote kile chenye thamani kubwa huwa hakipatikani kirahisi.Mafanikio yoyote yana gharama.Na vitu hivyo vitatu nilivyovielezea ambavyo ni; mawazo,muda,na nguvu ndizo gharama pekee unazopaswa kuzilipa ili kufanikiwa.na kwa kulipa kwako gharama hizo kutakufanya uwe vile unavyotaka kuwa
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment