Mambo 5 yatakayokusaidia Uweze Kufanikiwa Katika Maisha yako

Je una shauku ya kutaka kuongea na Mungu moja kwa moja? Ili akupe majibu yako kwa habari ya maisha yako?! fuata kanuni hizi ili uweze kufanikiwa moja kwa moja katika mambo unayoyafanya au unayotaka kufanya:

1. Kuwa mtu wa kusamehe, usipende kubeba vinyongo vya kutowasamehe wengine, kwani kufanya hivyo kuna kuweka katika mazingira ambayo kimisingi utashindwa kufanya mambo yako na kijamii yaletayo mafanikio. Lakini pia kumbuka kama hautakuwa mtu wa kusamehe pia hata wewe utashindwa kusamehewa pia.

2. Ichukie dhambi na uiache  kabisa, kuwa mtu wa toba, jikague moyo wako na matendo yako kila siku, omba rehema za Mungu unapoona umeenda kinyume na maagizo yake.

3. Acha tabia ya kuwasengenya na kuwasema  watu na watumishi wa Mungu, wapende na uwaombee, maana siyo kazi yako kuhukumu. Wapende na wengine, mtu akikosea muite muonye kwa upendo na umuombee acha tabia ya kusengenya wenzio, unajichelewesha.

4. Kuwa mtu wa maombi, maana yake siyo kila siku ushinde umejifungia, hapana kuwa mtu wa maombi ni kutafakari matendo makuu ya Mungu kila wakati, acha kuwaza ujinga na uovu.

5. Tenga Muda maalumu wa kuongea na Mungu wako. (muda wa maombi) na kutafakari neno lake.

Mpaka kufikia hapo hatuna jambo la ziada, tunakutakia utekelezaji mwema
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment