Fanya Uwekezaji kwa Wale Uwapendao/Ndugu/Marafiki na Jamii. Huu ni uwekezaji kwa wale unaowapenda na kwa jamii inayokuzunguka. Hapa kwa wewe ambaye una mke/mume/Watoto/ndugu na marafiki utapaswa kufanya kitu kwa ajili yao.
Kwa kupitia kuwekeza kwa hawa watu miaka ijayo utakuja kuyaona matunda ya uwekezaji wako. Utazungukwa na jamii ambayo inatokana na uwekezaji wako kwao. Utaishi Maisha ya furaha kwasababu uliweza kuitengeneza jamii ambayo ulikuwa unaitaka.
Mke/mume/Watoto hawawezi kuwa vile unavyotaka kama wewe hujachangia. Badilisha kile unachowekeza kwao kila siku. Maneno yako unayoongea nao ni uwekezaji, vile unavyowatendea ni uwekezaji miaka michache ijayo watakuwa kile ulichokuwa unawafanyia.
Sasa jiulize wewe umepambana tu kuwekeza kwenye fedha ukaisahau jamii, kukaibuka kizazi cha watu katili sana. Hawa watu watakuja kukudhuru wewe au wale unaowapenda. Lakini ukiwekeza japo kwa kuwaonesha upendo na kuwajali utajiepusha na madhara.
0 comentários:
Post a Comment