Vitu Muhimu Katika Chakula cha Kuku

Kuna vitu vitano muhimu vinavyotaijika kwa kuku ili awe na afya bora. Navyo ni kama vifuatavyo,

1. Protini
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kukuza mwili navyo ni kama ifuatavyo, Mtama, Dagaa, Alizeti na Soya. Hivi vyote inategemeana na maeneo uliko, nini kinapatikana kwa urahisi.

2. Wanga.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake ni kuupa mwili nguvu. Navyo ni kama ifuatavyo; mahindi yaliyo balazwa, pumba ya mahindi na pumba ya mpunga.

3. Mafuta.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kuupa mwili joto pamoja na kulainisha mmeng'enyo wa chakula mwilini. Kundi hili kuna vitu vifuatavyo; mashudu ya alizeti na mashudu ya pamba.

4. Madini
Hapa kuna madini ya aina mbalimbali ambayo kazi yake kubwa ni kuimarisha mifupa na ganda la juu la yai pia. Na haya madini ni muhimu sana, kwa sababu yanakazi kubwa katika mwili wa kuku. Yanamwezesha kuku kutembea vizuri na kwa ukakamavu.

Pia yai la kuku ili liwe imara lenye ganda gumu lazima apate madini ya kutosha. Bila kusahau madini yanasaidia kuku kutonyonyoka manyoya yake. Madini hayo ni kama ifuatavyo, mifupa, Chokaa ya kuku,  D.C.P hizuia kudonoana, kula mayai, maganda malaini. Pia uimarisha maganda ya mayai, husaidia kuongeza mayai.

5. Vitamini.
Ni aina ya vyakula ambavyo vinapatikana sana kwenye mbogamboga, lakini kazi yake kubwa ni kuimarisha mwili uwe vizuri kama vile kuona, kuwa na manyoya imara na afya bora. Kundi hili linavyakula kama vifuatavyo, mchicha, chainizi, spinachi na majani ya mpapai.

KUMBUKA:
Pia katika maduka ya mifugo kuna vitamini zinauzwa ambazo hutumika pia kama mbadala wa mazingira yetu yalivyo kuna baadhi ya maeneo kupata mbogamboga ni changamoto. Kuna "vitalyte" ni nzuri kwa kuku na hata nyingine pia
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment