Mambo muhimu ya Kufahamu katika Ujenzi wa Banda la kisasa la Kufugia Kuku


Yafatayo ndiyo mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kutengeneza banda bora la kufugia kuku;

Sehemu za kutagia (kama ni kuku wa mayai au wa kienyeji).
Katika banda bora la kuku wanaotarajiwa kutaga inapaswa kuwepo na sehem za kutagia zijulikanazo kwa jina la viota. Viota vinaweza kutengenezwa kwa mtindo wa kuku mmoja mmoja au ushirika.

Sehemu ya kutembelea.
Ni ukumbi mkubwa kulingana na idadi ya kuku, ambao ndani yake kunakuwa na vyombo vya maji na chakula, pamoja na kuku wenyewe.

Sakafu
 Zipo aina mbalimbali za sakafu kama ifuatavyo:-
    a) Sakafu ya saruji
Ni vema zaidi ukajenga sakafu ya saruji kisha ukaweka maranda juu yake ili kuzuia ubaridi unaotoka sakafuni, na vilevile kupata wepesi wakati wa kufanya usafi.

     b) Sakafu ya udongo au mawe
Jaza udongo wa mfinyanzi au mawe kisha siliba vizuri acha pakauke mwisho weka maranda kwa wingi.

     c) Sakafu ya chaga
Banda hujengwa kisha huwekwa chaga umbali wa futi mbili kutoka chini, chaga inaweza ikawa ya banzi, "chicken wire" au fito ili kuruhusu kinyesi cha kuku kudondoka choini.

Ukuta 
Unaweza kujenga ukuta kwa kutumia nguzo, pamoja na mabanzi au fito kisha kuzibwa vizuri na kuacha sehemu kubwa kwa ajili ya madirisha. Pia unaweza kutumia tofali za kuchoma, saruji au tofali za udongo kwa kujengea na kuacha sehem kubwa kwa ajili ya madirisha.

Paa
Vifaa vya kuezekea vinaweza kuwa ni vigae, nyasi, makuti au bati
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment