Mambo ambayo Hupaswi Kuwashirikisha Wateja wako katika Biashara Yako

Ni matumaini yangu kwamba wewe unayesoma hapa ni mfanyabiashara kwa namna moja au nyingine na ndio maana upo hapa au unasoma hapa. Kama mmiliki wa biashara au kampuni bila shaka yeyote ile unapendelea kushea/kuwashirikisha wateja wako mambo mbalimbali na hili hasahasa limekuwa ni jambo la kawaida sana katika Ulimwengu wa leo wa mawasiliano ya kisasa katika mitandao ya kijamii, karibu kila mtu usipomkuta facebook, basi utamkuta Insta, Twitter au mitandao mingineyo.

Kuwashirikisha mambo mbalimbali hakuwasaidii tu wateja wako lakini pia kunakuweka wewe mwenyewe katika nafasi ya juu zaidi kama mtu wa kutegemewa. Hata hivyo wafanyabiashara na wajasiriamali wengi hulifanya jambo hili kupita kiasi na kusahau kumbe kuna hatari mbalimbali pia zinazoweza zikajitokeza endapo watawashirikisha wateja wao mambo mengi kupitiliza.

Bila kupoteza muda wako mwingi hebu basi tukazione hizo siri 5 zikoje;

1. Maswala yako ya kifedha.
Usipende sana kulialia umasikini mbele ya wateja wako wala kujitapa kuwa una pesa nyingi(ukwasi), unapofanya mambo haya 2 kupitiliza  yanaweza kuwafanya wateja wako kukaa mbali na wewe kwani wanaweza kuhisi mambo mawili, kwanza wanaweza kufikiria biashara yako inachungulia kaburi(inafilisika) au pengine bei unayowatoza ni kubwa kupita kiasi. Hivyo utaona wakikimbia mmoja baada ya mwingine.

2. Masuala ya ndani ya biashara yako.
Wateja hawana haja ya kuyajua matatizo yako na wale wanaokusambazia mzigo, wala kujua matatizo yako na mwenye nyumba ulikopanga fremu ya ofisi/duka lako.

3. Matatizo ya wafanyakazi wako.
Kutoa malalamiko juu ya wafanyakazi wako kwa wateja wako hakuwezi kusaidia kitu, sanasana kutazidi kukufanya uonekane kama kwamba wewe ni mtu mbaya na mwenye roho mbaya. Ikiwa mfanyakazi wako ataboronga hata iiwa ni mbele ya wateja basi wewe cha kufanya kama bosi ni kuwataka radhi wateja kwa kosa hilo kisha rekebisha tatizo lililotokea halafu sasa njoo baadae ushughulike na mfanyakazi wako wakati mkiwa wenyewe wawili tu bila mtu mwingine.

4. Hali halisi ya soko ilivyo.
Kila mtu na si wewe tu hata na wateja wenyewe kuna wakati wanahisi hali ya kiuchumi kuwa ngumu. Hivyo usitegemee sana huruma toka kwao kwa kulialia kuwa ‘vyuma vimekaza, vyuma vimekaza’. Utawafanya wakushangae bure badala ya kukuonea huruma.

5. Kuhusiana na wateja wengine.
Kila mteja angependelea kujihisi kama yeye ndiyo mteja pekee, hivyo si vizuri hata kidogo kushea kupita kiasi stori za ni nani anayenunua kwako,ananunua nini,  ananunua kiasi gani na ananunua kupitia njia zipi. Sisemi ni vibaya kwa mfano kuweka ushuhuda(Testimonies) katika ukurasa au page zako lakini, fanya hivyo kimkakati na pia kwa kiasi
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment