JAMBO MUHIMU LA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUANZISHA BIASHARA YOYOTE ILE

Muungwana Blog ni sehemu sahihi sana kwako kuendelea kupata kile kilichokuwa bora zaidi kwako. Noamba nikualike rasmi siku ya leo ili tuweze kujufunza kwa pamoja jambo muhimu la kuzingatia unapotaka kuanzisha biashara yenye maisha marefu.

Ndugu naomba ufahamu ya kwamba kila biashara inayoanzishwa leo kama muanzisha biashara hiyo hatakuwa makini baishara hiyo itakufa baada ya miaka mitano ijayo. Najua utakuwa umeahangaa baada ya kusoma jambo hilo, ila nataka kukuambia huo ndio ukweli halisi.

Baishara nyingi hufa baada ya miaka mitano tangu zilipoanzishwa hii ni kwa sababu kumekuwapo na changamoto nyingi katika kufanya biashara kama mfanyabiashara huyo hatokuwa makini.

Hivyo kila wakati kabla ya kuanzisha biashara yeyote ile ni lazima mfanyabiashara huyo aweze kutambua ya kwamba ili kufanzisha biashara yenye maisha marefu, wakati wa kuchagua eneo la kufanyia biashara ni lazima mfanyabiashara huyo uweze kuchagua biashara zenye mahusiano na wafanyabishara wengine.

Kwa mfano kama kuna mtu anafanya biashara ya kuosha magari eneo fulani wewe unaweza ukanzisha biashara ya mgahawa, yaani wakati mteja anasubiri gari yake anaweza akawa anaendelea kula chakula katika mgahawa wako ambao umeujenga karibu na hiyo car wash.

Au unaweza ukaanzisha biashara ya kuuza matunda karibu na stendi za mabasi. Kufanya baishara kwa kuangalia mfano wa kibiashara  kunamfanya mteja akija eneo fulani kupata huduma mbili kwa wakati mmoja.

Hivyo kama unataka kufanya biashara fulani wakati wa kuchangua wazo la biashara hakikisha unachangua wazo ambalo litakuwa na muingiliano au mahusiano  na biashara zingine katika eneo husika.

Na: Benson Chonya
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment