JIKWAMUE KIUCHUMI NA KILIMO CHA MA APPLE

Tufaa ni tunda moja maarufu duniani ambalo hupendwa kuliwa na watu wa jamii zote, hii inatokana na utamu wake pamoja na faida za kiafya zinazopatikana kwa kula matufaa. Matunda haya hustawi zaidi kwenye nyanda za juu ambako joto sio kali, sehemu kama lushoto, Arusha, miteremko ya Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Njombe, Songea nk. Udongo ni wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji ndiyo ufaao kwa kilimo hiki.

Unaweza kupanda kwa kutumia mbegu au kwa kununua miche bora kutoka kwenye taasisiza kilimo. kama utatumia mbegu basi ni bora kununua mbegu bora au ukikosa mbegu basi jaribu kutumia zile utakazopata kutoka kwenye tunda lenyewe

Kama utachukua  mbegu za kwenye tunda basi zikaushe kwenye jua kwanza mpaka zikauke kabisa, zile za kukununua huwa zimekauka kwa hiyo huna haja ya kuzikaushatena.

Chukua karatasi laini (napkins/tissues) iloweshe maji kiasi kidogo kisha chukua mbegu zako na uzifunge na  karatasi hii vizuri kisha ziwekwe kwenye jokofu kwa kiasi cha wiki 3-4 zitaanza kuota/kumea, kuziweka kwenye friji husaidia kuua vijidudu vya magonjwa ambavyo huenda vilikuwepo kwenye tunda au mbegu

Chukua mbegu yako na uipande kwenye mifuko au chombo kama ndoo, usipande kwenye vifuko vidogo maana mmea huu hukua mkubwa kiasi na wenye mizizi mikubwa kabla ya kupandwa. Mmea wako ukifikia ukubwa wa futi moja mpaka mbili ni kipindi kizuri kuuhamishia shambani.

Umbali wa shimo hadi shimo ni kiasi cha futi 15 mpaka 18 kutoka mti hadi mti. Hakikisha unapanda miche yako wakati wa mvua za kwanza, Mashimo yawe na kina cha futi mbili na upana futi 3. Weka kasi cha debe 1 la samadi au mboji na changanya vizuri na udongo.

kumbuka kuacha kisahani kwa ajili ya kukusanya maji ya mvua au unapomwagilia na utandaze majani/nyasi kiasi cha futi 3 kuzunguka mti wako, hakikisha wanyama kama mbuzi na ng'ombe hawaingii shambani na kula miti yako. Baada ya mwaka hutakuwa tena na haja ya kumwagilia miti yako kwani itaweza kukua yenyewe kwa kutegemea mvua

Wadudu na magonjwa
Wadudu wanaoshambulia zaidi mitufaa ni vidukari (moth) na pia ugonjwa wa madoa meusi (black spot) ndio unaoshambulia zaidi, ili kupambana na ugonjwa na wadudu hawa hakikisha unatuma kiutilifu chochote chenye pareto (pyrethrum) ndani yake.

Kuvuna
Uvunaji ni baada ya miaka mitatu lakini miche ya kuunga huanza kuzaa mapema hata ndani ya mwaka, ila nashauri usiruhusu matunda mengi kwenye miti midogo ili kuzuia matawi kuvunjika kwa hiyo punguza matunda kabla hayajawa makubwa na kubakisha machache
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment