Usikubali kutumia nguvu zako mwenyewe na kila kitu mwenyewe wakati kuna uwezekano wa kutumia wengine na ukafanikiwa. Jifunze ni kwa namna gani hicho unachokifanya sasa hivi ukiongezea kitu kutoka kwa wengine utaweza kufanikiwa Zaidi.
Usizitegemee akili zako mwenyewe, jifunze kwa wengine, muombe Mungu.
Usitegemee Nguvu zako mwenyewe, jifunze kuzitumia nguvu za wengine pia.
Usitegemee muda wako pekee jifunze namna ya kutumia muda wa wengine ili kuongeza uzalishaji wa haraka kwenye kile unachokifanya.
Usitegemee pesa zako mwenyewe jifunze namna ya kutumia pesa za wengine na kuzizalisha ili upate faida Zaidi.
Ipo siku utachoka, ipo siku utakuwa na majukumu mengi Zaidi hivyo ni muhimu kutengeneza mfumo wa kuweza kuwatumia wengine ili mambo yako yawe na uwezo wa kuendelea kwenda hata kama haupo. Iwe ni biashara au hata kipaji chako bado kuna namna unawahitaji wengine ili uweze kuwa na matokeo bora Zaidi
0 comentários:
Post a Comment