KANUNI ZA KUONGEZA FAIDA KATIKA UFUGAJI WA KUKU

Ufugaji kuku ni biashara kama biashara nyingine, kuna wafugaji wengi wanaingia gharama zisizo za lazima katika kufuga kuku hali ambayo inawapelekea kupunguza faida yao na mara nyingine hata kutopata faida kabisa, hali hii inawakwaza wafugaji na wengine hukata tamaa kabisa ya kufuga. Lakini hayo yanasababishwa na wao wenyewe wafugaji bila wenyewe kujijua.

Kupitia somo hili tutakumbushana ni namna gani mfugaji anaweza kuzikwepa gharama zisizo za lazima katika ufugaji ili aweze kupata faida mara dufu.

Zifuatazo ni kanuni za kuongeza faida katika ufugaji kuku:-

1. Kupata vifaranga bora
Vifaranga bora ni wale waliototolewa katika wakati uliopendekezwa kitaalaam hali ambayo inamjenga kifaranga kuwa na kinga asilia ya mwili ya kutosha, kwahiyo mfugaji anaweza kufuga hadi kufikia kuuza bila kutumia dawa za kutibu ugonjwa wowote zaidi ya chanjo na dawa za kuanzishia tu, hivyo ataokoa pesa nyingi za kumuita daktari na kununua madawa na faida itaongezeka siku hadi siku.

2. Uleaji mzuri (proper management)
Hapa tunakusudia uasafi wa banda, vyombo vya chakula na maji, maji ya kunywa na muhudumu mwenyewe. Kwan magonjwa mengi ya kuku yanasababishwa na uchafu, hivyo uleaji ukiwa mzuri magonjwa hayatakuwepo halikadhalika na na gharama za matibabu hazitakuwepo pia.

3. Chakula bora
Mfugaji anatakiwa ahakikishe anapata chakula bora kwa ajili ya kuku wake, chakula bora ni ambacho kimekingwa na magonjwa yote na kinakuza kuku kwa wakati, lakin pia chakula bora ni kile ambaho hakisababishi mazingira hatarishi katika banda kama vile kulowesha banda. Chakula ambacho kinalowesha banda kina hatari ya kusababisha magonjwa mbalimbali kama vile coccidiosis na typhoid, hali ambayo mfugaji ataingia gharama za kutibu mara kwa mara na kununua maranda.

4. Kupata soko la uhakika
Ili upate soko la uhakika ni lazima uwe na tabia ya kutafuta taarifa (search information), kwa kutafuta taarifa itakuwezesha kujua hali ya soko iliyopo ili nawe uweze kujipanga. Na kama ukiwa unategemea tu mtu wa tenga aje mara nyingi utakuwa unalalamikia soko, hali ambayo itakupa stress na kuuza kuku wako kwa bei ya hasara. Ila kama unajua hali halisi ya soko basi hata akija mtu wa tenga nyumbani hatokudanganya na utakuwa na uhakika na bei yako
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment