Kwa asili watu wengi hutamani kuona wanafanikiwa haraka katika jambo lolote ambalo watafanya, hata mimi na wewe ndani mwetu kuna hilo hitaji kama mambo yangeenda kama vile mtu ambavyo angetaka iwe.
Lakini ukweli kuhusu maisha ni kwamba maisha ni mchakato kwa hiyo kila kitu kinahitaji muda ili kuweza kukijenga na kufikia mafanikio ambayo mtu anatamani kufikia.Kuna mambo mengi ambayo tulianza kwa mategemeo ya kufanikiwa haraka lakini matokeo yake imetuchukua miaka mpaka kuja kufikia hatua ambayo tulitamani itokee katika kipindi cha muda mfupi.
Watu wengi hupendelea kujifunza katika hatua ambayo tayari mtu amepata mafanikio, bila hata kujua kuwa unahitaji kujifunza hatua na njia mtu huyo alizopitia hadi kufikia mafanikio unayoyaona leo.
Karibu tena msomaji wetu katika mtandao wetu wa maishanifursa. Leo tutajikita katika mada ambayo nimeipa kichwa “hatua 4 za kuanza na kukua kidogo kidogo” Nakushukuru sana kwa kuendelea kufuatilia kazi zetu uwepo wako ni muhimu sana kwa kazi yetu kwani bila wewe kazi yetu haina maana.
Tamaa inabaki kuwa tamaa kitu ambacho hakiko halisi huwezi kukishika wala kukiona kwa macho ya mwili. Tamaa ni muhimu lakini ikizidi kiwango cha uhitaji basi hugeuka kuwa shida katika maisha.
Binadamu wameumbwa kutokupenda shida huku wakitamani sana maisha ya mkato kuliko njia ya kuzunguka. Ndio maana wengi wamenaswa na kupoteza pesa nyingi kwa kujiingiza kwenye shughuli ambazo waliahidiwa kupata matokeo ya haraka katika kipindi kifupi.
Ukitaka kupata wafuasi wengi nyakati za leo iwe ni biashara au huduma yoyote inayohusu uzalishaji basi wewe ahidi watu kuwa wakiwekeza kwa muda mfupi watapata faida na utajiri wa haraka bila kutoka jasho sana.Basi nakuambia kipindi cha muda mfupi utakuwa na umati mkubwa wa watu ambao wanakufuata wapate mafanikio kwa njia ya mkato.
Japokuwa kila binadamu amepewa akili na ufahamu wa kutosha ili aweze kuchambua jema na baya, ukweli ni kwamba katika mazingira ya ahadi ya kupata faida haraka watu huwa hawapendi kujihangaisha kabisa kufikiri,kuhoji na kujiuliza maswali matokeo yake wengi wameingia kwenye msongo mkubwa wa mawazo baada ya kupoteza.
Kutokua na taarifa sahihi juu ya ukweli halisi unaoendesha maisha ni janga ambalo limesababisha watu wengi kupoteza na kupata hasara kubwa katika maisha zamani hizi na hivyo kujifunza kwa maumivu makubwa.
Kuna waliokuwa na fedha wakaingia kwenye biashara wakitarajia kupata mafanikio ya haraka, lakini matokeo yake wakajikuta wanapoteza hata fedha kidogo walizokuwa nazo na kubaki hawana hata kitu kidogo cha kuonyesha.
Wengine waliingia katika biashara ya kilimo kwa mategemeo ya kubadilisha maisha kwa muda mfupi, lakini kumbe hawakuwa na taarifa sahihi wakajikuta wanapokeza kinyume na matumaini yao.
Wengine walistaafu na kupata pesa ya mkupua busara ikawatuma kuanza kujifunza kufanya biashara ambazo hata wakiwa na nguvu hawajawahi kujaribu kuzifanya,hawakufika mbali pesa ikawa imekwisha na kubaki wakiw wamekula mbegu yote hawana tena cha kupanda.
Mifano ya watu walioanza wakitazama upande mmoja tu wa sarafu kwa matumaini makubwa ya faida bila kuwa na taarifa sahihi ipo mingi na pengine hata wewe unayo ama inayokuhusu ama uliyoshuhudia ikitokea kwa watu walio karibu yako au majirani zako.
Kila hatua ya mafanikio ambayo mtu amefikia iwe ni biashara, huduma, ndoa au familia n.k chunguza kwa undani utagundua kuwa nyuma ya hayo mafanikio kuna hadithi kubwa ya kuvutia ambayo ni mchanganyiko wa matamu na machungu.Yote ni viungo muhimu katika kukamilisha ladha halisi ya maisha.
Hicho kipande cha hadithi cha matamu na machungu kabla ya mtu kufikia mafanikio ndilo somo muhimu sana ambalo watu wengi tunakosa kupata nafasi ya kujifunza kabla hatujaanza safari kuelekea mafanikio.
Nataka kukushirikisha mambo muhimu manne kwa uzoefu wangu ambayo ukiyafuata naamini yanaweza kukusaidia ama kuanza vizuri kama ulikuwa hujaanza au kuendelea vizuri kama tayari umeanza lakini ungependa kuwa na taarifa ambazo zitakusaidia hatua kwa hatua kufanya.
1. Wekeza kwako kwanza
Tuseme tayari umekwishavuka ile hatua ya kutafuta biashara au shughuli ya kufanya yaani unalo wazo kichwani tayari, lakini unataka kuanza unasita kwa kuwa hujui uanzie wapi. Mahali pazuri pa kuanzia ni wewe kufanya uwekezaji kwako mwenyewe kabla hata ya kuanza kuwekeza moja kwa moja kwenye wazo lako. Tafuta elimu binafsi itakayokusaidia kupata maarifa ya kutosha kuendesha au kufanya shughuli unayotaka kufanya.
Kurukia kufanya shughuli yoyote kwa kuiga bila kuwa na maarifa ya kutosha kuhusiana na biashara au shughuli hiyo unayotaka kufanya ni sawa na kuruka ngazi badala ya kukanyaga hatua moja baada ya nyingine kwenye ngazi.
Watu wengi katika hatua hii hupenda kurukia moja kwa moja kwenye kuanza biashara au shughuli bila hata kutafuta maarifa kumsaidia kuanza vizuri. Njia za kupata maarifa ziko nyingi katika zama hizi za kizazi cha sayansi na teknolojia. Ni rahisi kujifunza kutoka kwenye mtandao wa intaneti chochote unachotaka kujifunza na kupata maarifa ya msingi. Hudhuria semina na makongamano. Soma vitabu au tafuta mtaalam katika hilo eneo unalotaka kuingia akusaidie.
Hapa simaanishi kwamba lazima uende chuoni uwe mtaalam katika eneo uliloamua kujikuta ndipo sasa uweze kuanza: hapana ni hatua ya kujipatia ufahamu wa msingi kukuwezesha kuanza ili uendelee kujifunza kadri unavyoendelea. Hakuna wakati utakua umejifunza kila kitu katika jambo lolote utakalofanya.
2.jifunze kutoka kwa wanaofanya
Kuna tofauti kubwa ya kujifunza kutoka kwa mtu anaefanya na mtu anaefundisha tu bila kufanya. Yapo maarifa mengi unayoweza kuchota kutoka tu kwa mtu ambaye tayari anafanya kitu ambacho na wewe unataka kufanya ambayo huwezi kupata shuleni au chuoni.
Utapata kujifunza magumu na machungu aliyopitia hadi kufika mahali alipofikia. Siku ambazo alikutana na magumu moyo ukainama alifanya nini hata kuinuka tena. Hadithi yake ya mafanikio alikotoka kuanzia mwanzo mpaka kufikia mahali alipo leo ndilo somo la muhumu unalopaswa kujifunza kutoka kwa waliotangulia kufanya unachotaka kufanya.
Kama ni mtu wa kupanga matumizi ya muda wako kabla hata hujautumia basi unaweza hata kuomba kazi ili uwe ndani hata kama kwa kulipwa mshahara mdogo kwa sababu lengo lako siyo pesa ila ni kujifunza.
3. Anza kidogo kidogo
Ni vizuri sana kuwa na ndoto kubwa ambayo utaanza kuitekeleza kidogo kidogo hatua kwa hatua. Sasa unahamisha yale maarifa nadharia uliyokuwa nayo na kuweka kwenye vitendo sasa. Yapo mambo mengi ambayo utajifunza kupitia hatua hiyo ya kuanza kwa hiyo utahitaji marekebisho ya mara kwa mara bila kuathiri kule unakotaka kufika kupitia biashara, huduma au biashara unayofanya sasa.
Kuna makosa mengi utafanya kadri unavyoendelea na hayo yanakusaidia jinsi unavyoyashughulikia hubaki kama ulivyokuwa unapata upata uzoefu wa kutosha.
Kidogo kidogo utakuwa unawekeza zaidi kadri ya elimu unavyoendelea kuipata kupitia hatua ya uendeshaji. Kila siku inayopita utakuwa umeongeza kitu cha kukusaidia biashara yako na mwenyewe kukua. Kwa utaratibu huu sitashangaa kama siku moja biashara yako itakua kubwa ili mradi tu hukuruka hatua yotote.
4. Jipe muda wa kutosha
Kama umefuatilia vizuri tangu mwanzo nimesisitiza sana habari ya muda. Hiki ni kigezo muhimu sana katika hatua yoyote ya mafanikio. Usisahau kwamba pamoja na hatua zote zilizotangulia kuzipita, unahitaji kujipa muda wa kutosha kabla ya kuanza kuona mafanikio.
Unahitaji angalau kutenga muda kati ya mwaka mpaka miaka mitatu ya mchakato kuisimamisha biashara yako kabla ya kuanza kuona mafanikio. Ikitokea chini ya muda huo ukafanikiwa haidhiru chochote cha msingi ni kutokuwa na matarajio ya kufanikiwa haraka haraka. Hakuna njia ya mkato kwenye mafanikio. Maisha ni shule iliyo jaa mlolongo wa mitihani mingi ya kustukiza katika kila hatua ya maisha unayopiga.
Hiki ndicho kilichokua kinalia ndani mwangu leo nilichotamani kukushirikisha. Namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi hii ya kukuhudumia nikiamini itakusaidia kukuvusha kutoka mahali fulani hadi mahali fulani.

Naamini utakuwa umepata kitu kupitia makala hii fupi. Ukiwa na uhitaji wowote au ushauri katika eneo lolote la kuboresha maisha,biashara yako au hata una wazo kuanzish kitu fulani lakini unakwama;usisite kuwasiliana nasi kupitia njia za mawasiliano hapo chini. Aidha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno, whatsapp kupiga simu au kututumia barua pepe nasi tutarudi kwako mapema iwezekanavyo.Tutashukuru kama watakaotutafuta wakiwa ni wale ambao kweli wanamaanisha
0 comentários:
Post a Comment