Jinsi ya kukuza Mifenesi na manufaa yake


Mmea wa fenesi unaweza kustahimili viwango vya juu vya joto na baridi. Mfenesi uliokomaa unaweza kustahimili joto la hadi digrii 48 na baridi ya hadi digrii 0. Baadhi ya mifenesi hukua hadi urefu wa futi 100, lakini pia kuna aina zingine ambazo hukua hadi urefu wa futi 10-20.



Mti huu unaweza kuzaa matunda kwa zaidi ya miaka 100. Ni mmea wa kipekee kwani kati ya matunda yote duniani, ndio unazaa matunda yenye uzani wa juu zaidi wa kilo 50.


Kwa nini upande mifenesi?
Huu ni uwekezaji wa muda mrefu labda kwa maisha yako yote. Sehemu zote za mmea huu zina manufaa tele. Pia ni mti unaoweza kumpa mkulima kivuli nyumbani na kuwapa ndege makao. Mfenesi mmoja unatosha kuwapa matunda kijiji kizima huku pia ukikupa hela.
Mbinu za kupanda
Miche ya mfenesi inaweza kutengenezwa kutokana na vipandikizi lakini mbinu hii imewapiga chenga wakulima wengi. Hivyo, mbinu ya kukuza kutokana na mbegu huwafaa wakulima wengi. Unatakiwa kuteua mbegu kubwa kutokana na fenesi lililoiva vizuri na kuziosha kwa maji yenye kiwango kidogo cha joto.
Sasa unaweza kupanda mbegu hizo katika kitalu kisha kuhamisha miche shambani. Unaweza pia kununua miche kutoka kwa wapanzi wa miche, ila watapatikana katika maeneo ya Pwani ya Kenya na pia kaunti ya Kakamega hasa mjini Mumias.
Iwapo uko mbali na maeneo haya unaweza kumtuma mtu akununulie fenesi lililoiva vizuri ili baadaye upande mbegu zake na kukuza miche yako mwenyewe.
Jinsi ya kupanda
Chagua eneo pana lililo wazi na linalopata jua kwa wingi, ondoa magugu na uchimbe shimo. Ili kuhakikisha maji yanapenyeza bila matatizo, changanya mbolea ya kawaida, majani, changarawe na mchanga wa shamba lako na kutia mle shimoni.
Sasa unaweza kupanda mche mmoja wenye afya nzuri ndani ya lile shimo. Nyunyizia maji na ufunikwe kwa nyasi ili kuzima unyevunyevu kuyeyuka kwa hewa.
Kama unapanda mche uliopandikizwa, usifunike majani yake ya juu maanake mmea utaoza kutoka ndani na kukauka. Tenganisha mimea kwa mita 10 kwa 10.
Mwagiliaji na uwekaji mbolea
Mfenesi hukua vizuri katika maeneo yenye joto ambayo hupata mvua ya kutosha. Hii inmaanisha utahitajika kuunyunyizia maji kila mara sababu unahitaji mazingira yenye unyevunyevu na mchanga laini. Hata hivyo, epuka kunyunyizia maji kupita kiasi hasa katika miaka yake miwili tangu kupanda.
Mara moja kwa mwaka, hasa mwanzoni wa mwezi Julai au Agosti, ongeza mbolea ya zizini kwa mmea ili kuupa nguvu. Unaweza kutia fatalaiza iliyosawzishwa, mara mbili kwa mwaka. Ukifikisha miaka mitatu, unaweza kutia fatalaiza ya kiwango cha 8:3:9.
Kutunza
Weka nyasi kuzingira mmea wakati baridi imekaribia kufikia kiwango cha digrii 0 ili kulinda mizizi ndidi ya baridi hiyo.  Mara kwa mara ondoa matawi ya ziada kuhakikisha urefu wake umesalia kuwa futi 20.
Wakati mmea umezidisha urefu wa futi 12, kata upande wa juu wa shina lake hadi futi 8 ili kuuwezesha kupata matawi mengi. Mfenesi hukomaa baada ya miaka 3-6. Katika wakati huu, mfenesi ukichanua maua ya kwanza, yaondoe ili uendelee kukua.
Mara moja kwa mwezi ondoa magugu yaliyo karibu na mmea kwani yataanza kutumia madini muhimu yanayohitajika na mmea huu.
Funika eneo la mizizi kwa nyasi wakati wa kiangazi ili kuhifadhi unyevunyevu na kuepuka magugu kumea.
Kuvuna
Kati ya miaka 3-6 baada ya kupanda (kutegemea na utunzaji na mazingira uliyopanda) mfenesi huanza kuchanua maua na baada ya miezi 2-3, mafenesi madogo ya rangi ya kijani kibichi yanaweza kuchumwa kutumika na wapishi.
Matunda yaliyokomaa huwa tayari kuvuna baada ya miezi 4-5 tangu maua yachanue. Wakati huo mafenesi huwa na harufu ya kupendeza na ngozi yake hubadilika kutoka kijani kibichi kuwa manjano.
Mfenesi huzaa matunda nyakati zote za mwaka ila katika maeneo mengi duniani, linavunwa sana katika msimu wa kiangazi
Wadudu na magonjwa
Baadhi ya wadudu wana mazoea ya kuvamia mfenesi na kuyatoboa mashimo yakiwa mtini huku pia nao ndege wakifurahia maji yake matamu na kuharibu matunda.
Wadudu wanaotoboa mashimo huathiri sehemu zote za mmea, lakini ukiwapulizia dawa ya kujitengezea nyumbani isiyo na kemikali huweza kuwaua na kuwazuia. Pia kuufunika mmea wakati matunda yamekomaa kutasaidia kukinga matunda dhidi ya ndege hatari.
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment