Mambo ya kuyatizama ili kuongeza thamani katika Biashara yako

Huenda ukawa anafanya biashara au unapenda kufanya biashara lakini yapo baadhi ya mambo ya msingi ya kuyatazama kabla  au wakati wa kufanya biashara. Tupo baadhi yetu tunashindwa kufikia malengo yetu hasa katika kuwaza au kupoifanya biashara. Leo katika makala haya nitakwenda kukueleza juu ya kujijengea misingi ili kukuza  na kuongeza uthamani wa biashara.

Biashara yeyeto ile endapo itafanya kwa misingi ambayo inafaa itakuwa na faida sana. Zipo baadhi ya biashara hazikui kwa sababu  ya kuzifanya biahara hizo miaka yote kwa staili moja. Kama kweli unataka kukuza biashara yako ni lazima utazame ni kwa jinsi gani unaweza kubadilisha mfumo wa kiutendaji ambao utakufanya uweze  kupata faida zaidi. Biashara hata kama itakuwa ndogo au kubwa kiasi gani endapo utaifanya kwa ubunifu na umakini wa hali ya juu utaongeza wateja zaidi.

Yafuatayo ndio mambo ya msingi ya kuongeza uthamani wa biashara ili kuongeza wateja zaidi;

Ladha na  fasheni.
Kimsingi kuna baadhi ya watu huwa tunafanya biashara tu bila kuangalia vitu kama  vile ladha  au fasheni (mitindo inayokwenda na wakati) . huenda ukawa haujanielewa ngoja nikupe mfano kama wewe unafanya biashara angalie wateja wako wanakula au wanakunywa kwa sababu ya kukidhi mahitaji au kwa sababu wanaridhika na kile wanachokula au kunywa. Kama wewe unafanya biashara nyingine kama vile, nguo, viatu, magari, vitu vya ujenzi vitu vingine ni lazima uangalie vitu vinavyokwenda na wakati , kwani endapo utafanya hivyo ndivo vitavyokufa uongeze wateja. Tukumbuke ya kuwa kadri vitu vinavyokuwa vya fasheni ndivo wateja wabavozidi kuwa wengi.

Kipato cha wateja.
Katika kutazama ni vipi unaweza kuongeza uthamani wa biashara jambo la msingi ni kujua kipato cha wateja wako.  Kama eneo ambalo unaishi wateja wako wanaoishi ni watu wa kipato cha kawaida ni lazima ujue ya kuwa bidhaa na bei lazima vilingane na wateja wako mfano huwezi kwenda kuanzisha biashara ya super market kijijini. Pia tukumbuke ya kuwa kuna baadhi za bidhaa endapo bei zitakuwa chini ndio huwa zinawateja wengi zaidi, halikadhalika kama wateja wako ni watu wa kipato cha juu basi bidhaa na bei ya bidhaa zako ni lazima yakidhi mahitaji ya watu hao kwa namna moja au nyingine.

Uhitaji wa bidhaa.
Katika biashara ni lazima uangalie uhitaji wa bidhaa au huduma kwa wateja wako. Kanununi za kibiashara zinasema kwamba kama kama bidhaa  zina gharama ndogo za uzaji uhitaji wa wateja hua mkubwa sana na kinyume chake inawezekana pia. Pia ni lazima usome soko lako kwa maana ya kuangalia wateja wako wanahitaji nini, na ujalibu kuchua mahitaji yao na kuwahudumia bidhaa hizo ili kukidhi mahitaji yao.

Matangazo
Matangazo husiana na jinsi ya upatikanaji na matumizi ya bidhaa au huduma husika. Ili kuwavutia wateja juu ya biashara yako ni vyema kuitangaza bidhaa yako ili kuwafanya  wateja waweze kuitambua biashara ambayo unaifanya. Katika kuitambulisha bidhaa katika matangazo ni lazima uwe mbunifu ili tangazo linapomfikia mtumiaji ahisi yeye ni sahemu ya biashara hiyo kwa maana ya kwamba mtumiaji aseme bila bidhaa hawezikuishi.

Hali ya hewa.
Biashara ni yeyote ni lazima ujue ni kipindi gani bidhaa yako itauzika zaidi. Biashara zingine ni za msimu kwa mfano kama unauza miavuli najua utaifanya kwa nguvu zaidi kipindi cha mvua. Hivyo kwa kuwa wewe ndo unataka kuifanya biashara au umekwisha kuanza biashara ni lazima uzingatie je biashara yako  itauzika zaidi msimu gan? Ukizingatia hayo, biashara yako iatakuwa ni yenye faida kubwa.

Kama unataka kufanya biashara au unafanya biashara na unataka kupata faida kubwa ni lazima uzingatie hayo kwa namna moja ama nyingine.

Na; Benson Chonya
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment