Karibu tena mpenzi msomaji wa blog hii, nadhani mpaka sasa umeweza kupata angalau mwanga wa kujua na kuilinda biashara yako ili iwe yenye tija na yenye kukua kila siku, leo nitakwenda kuzungumzia hasa aina za biashara ili kukuwezesha kujua ni aina gani hasa ya biashara unafanya.
Biashara za huduma, (Service Business)
Hizi ni aina ya biashara ambazo hujishuguisha na mauzo ya bidhaa zisizoonekana wala kushikika mfano; huduma za elimu, afya, ushauri wa kitaalamu, ambapo katika biashara hii pia imegawanyika katika sehem kuu tatu pia
Huduma za Kitaalamu mfano sharia, ushauri wa maswala ya fedha n.k
Huduma za Kifedha(Financial Service) mfano; bima, benki
Huduma za Mawasiliano (Information Service)
Biashara ya kuuza bidhaa (Merchandise Business)
Hizi ni aina za biashara ambazo hujishugulisha na kununua bidhaa kwa jumla na kuuza kwa rejareja, bidhaa hizi ni lazima ziwe zinashikika na kuonekana kwa macho, aina hii ya biashara ni maarufu kwa jina la “BIashara za kuuza na kununua”
Biashara mseto (Hybrid Business)
Hizi ni aina za biashara ambazo zinakuwa zimechangamana kwa pamoja, biashara hizi huusisha pande mbili ambazo ni utoaji wa huduma na kwa muda huohuo huuza bidhaa kwahiyo mmiliki wa biashara hii inaweza kutumia huduma ambazo hazimwingizii faida ila huku akiwa anauza bidhaa ambazo zitakuwa zinamwingizia faida. Mfa; unaweza ukawa unafanya biashara ya kuuza dawa za binadamu ila kwa wakati huohuo unatoa bure huduma ya ushauri wa maswala ya afya, kumbuka wapo watu ambao wao wanauza dawa tu pia wapo ambao wamejikita katika ushauri wa kitaalam juu ya afya, kwa hiyo utakuwa unapata faida katika kuuza dawa ila ile huduma ya ushauri unatoa bure
0 comentários:
Post a Comment