Zijue Mbinu za Kupanga Bei katika Biashara yako

Mara kadhaa nmekuwa nikieleza ya kwamba ifike pahala tuache kufanya biashara kimazoea kwani dunia ya sasa inaenda kasi kuliko neno lenyewe, hivyo hatuna budi tufanye juhudi za hali na mali kuweza kuendana na kasi hiyo.

Kwani siri kubwa ya ushindi wa kibiashara nikuweza kujifunza kila iitwayo leo hususani masuala ya kibishara. Usikate tamaa kujifunza na karibu sana tujifunze kwa pamoja.

Moja ya changamoto kubwa ambayo huwakunga wafanyabishara wengi ni kwamba huwa hawajui ni jinsi gani ya kupanga bei katika biadhaa au huduma.

Na utakubaliana na mimi ya kwamba watu wengi hupanga bei kutoka na kumtazama mfanyabiashara mwingine anafanyaje, kufanya hivyo sio mbaya ila leo nitakuongezea mbinu zingine ambazo zitakusadia katika upangaji wa bei wa bidhaa au huduma ambao utakufanya ujitofautisha kivingine na wafanyabishara wengine na hatimaye kupata faida.

Zifuatazo ndizo mbinu za kupanga bei katika biashara;

1. Gharama za uendeshaji wa biashara.
Biadhara yeyote ili uweze kupata faida ni lazima ufanya mahesabu kwa kuangalia gharama za uendeshaji wa biashara nzima. Gharama hizo zinaweza zikawa ni za ununuzi wa bidhaa, gharama za usafilishaji na gharama kwa ajili ya ulipaji fedha kwa ajili ya kodi ya pango na serikali kama ipo.

Baada ya hapo angalia gharama zote ambazo zimetumika kisha angalia ni kiasi gani kitafaa kwa mteja kuweza kununua bidhaa au huduma hiyo.

2. Ushindani katika biashara.
Hii pia ni mbinu nyingine ya kuzingatia katika upangaji wa bei. Siku zote kumbuka kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara wengine wao huuza kwa gharama gani? Baada ya kupata majibu ndipo na wewe ujue katika biashara yako uweze kupanga bei.

Katika ushindani wa kibiashara usiangalie tu suala la bei kwa washindani wako bali angalia wao wanafanyaje biashara zao kiujumla na angalia ni wapi ambapo wanafanya makosa na wewe zifanye changamoto  kama fursa ambayo utaipatia majibu katika biashara yako ambayo itakupa faida kubwa.

3. Uhitaji wa bidhaa au huduma.
Mara zote mfanyabiashara ni saa, ndiyo ni saa wala usishangae huu ndio ukweli, maana yangu ni kwamba mfanyabiashara yeyote ni lazima ujue kusoma alama za nyakati zinavyokwenda. Alama za nyakati ndizo zitazokusaidia kupanga bei na kupata faida.

Kwa mfano ukiangalia bei za makoti na masweta msimu wa baridi na joto utagundua ni tofauti hii ikiwa na maana mahitaji ya makoti huwa kubwa zaidi msimu wa baridi hivyo bei huwa kubwa zaidi ukilinganisha msimu wa joto. Hivyo ili kuwa mshindi wa kibiashara usiyekuwa na manung'uniko katika biashara yako hakikisha unajua kusoma alama za nyakati.

Pia katika  kanuni ya kiuchumi inaeleza ya kwamba pale mahitaji ya watu katika bidhaa au huduma kuwa kubwa bei pia inaweza kupanda pia lakini kinyume chake inawezekana, pia  inawezekana  mahitaji ya watu kibiashara ikapungua pia kuna uwezekano mkubwa wa bei ya bidhaa au huduma kupungua.

Pia mara zote kumbuka ya kwamba upangaji wa bei hutazama kwa asilimia mia uhitaji wa bidhaa katika eneo husika.

Mwisho nimalize kwa kusema kila siku kaa chini na kutafakari  juu ya biashara yako husasani suala la kuongeza thamani ili kupata faida mara dufu.

Na; Benson Chonya
Share on Google Plus

About Admin

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comentários:

Post a Comment